Senin, 28 September 2009

In Swahili:Atimuliwa miss Tanzania kwa uja uzito


Mwakilishi toka mkoa wa Iringa kwenye Miss Tanzania 2009/10 Witness Nesphory ameondolewa kwenye kambi ya Maandali ya Miss Tanzania kutokana na kubainika kuwa ni mjamzito.

Kutoka katika chanzo chetu cha habari ndani ya kambi hiyo ilisemekana kuwa Witness ameonekana kuwa ni mgonjwa tangu alipowasili kwenye kambi hiyo na ameshindwa kujumuika na wenzake kufanya mazoezi mbalimbali yanayoendelea kujiandaa na shindano hilo.

Chanzo hicho kiliendelea kusema kwamba, Witness aliambiwa arudi nyumbani na viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania baada ya kuonekana kwamba hali yake kila siku inazidi kuwa mbaya licha ya kupatiwa huduma zinazohitajika.

Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, alithibitisha kwamba mrembo huyo amerudishwa nyumbani kwao kwa ajili ya kupatiwa matibabu ziadi.

Lundenga alisema kwamba lengo la kufanya hivyo lilitokana na mrembo huyo hali yake kutobadilika licha ya kupatiwa huduma za afya.

Aliongeza kuwa mara baada ya warembo kurejea jijini Dar es Salaam, wakitokea kwenye ziara ya vivutio vya kitalii katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara, Witness aliendelea kuumwa na kufikia kulazwa katika hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar