Senin, 28 September 2009

Mez B Kichapo Cha Mbwa


Moses Rubaga a.k.a Mez B usiku wa kuamkia weekend hii alipata kipigo cha hatari na watu wasiojulikana mara baada ya kusababisha ajali nje ya ukumbi wa Club 84 Mjini Dodoma.

Akiongea na Dar411 kwa uchungu kabisa Mez B alisema alikuwa akitokea Royal Hotel kwa bahati mbaya gari aliyokuwa nayo ikapata hitilafu zilizopelekea kuyavaa magari yaliyokuwa yamepaki eneo hilo.

“Ilikuwa ni bahati mbaya sio kitu cha kukusudia lakini nashangaa mara baada ya ajali jamaa walikuja kunivamia na kunipatia kipigo cha nguvu kilichopelekea kuvuja damu nyingi na maumivu makali” alisema Mez B ambaye alikuwa akiongea kwa maumivu.

Mez B amesikitika kutokana na kitendo hicho akisema hakutegemea kama wakazi wa mji anaotokea wangeweza kumfanyia kitu kama hicho ila yeye kama kawaida ataendelea kuwakilisha Dodoma kwani nyumbani.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar